Mshambuliaji chipukizi wa klabu ya Juventus Moise Biot Kean ambae jana alichezea timu ya Taifa ya Italia kwa mara ya kwanza akiingia dakika ya 62 kwenye mechi dhidi ya USA ana deni kubwa.
Deni hilo haliwahusu washabiki wa Juve wala klabu ya Juventus.
Ila deni hilo linamhusu Kean yeye mwenye kwa kauli yake alioitoa kwa Baba yake miaka kadhaa iliopita.
Kean alizaliwa tarehe 28 mwezi Februari mwaka 2000 hukoo Verselli nchini Italia.
Na kwa sasa ametambulika rasmi kuwa mtaliano baada ya kucheza mechi hio ya jana.
Mkimuona popote pale mwambieni akatimize deni lake.
Mzee Biorou Kean anamsaka mwanawe huyo popote pale na atakapo mkamata wakiwa wawili tu amsomee mashtaka.
Lakini mara zote ambapo Kean alipokutana na Mzee wake basi amekutana nae wakiwa na lundo la watu, kitu ambacho Baba yake hakitaki, na hayupo tayari kumsomea mashtaka penye hadhira.
Baba anataka kumbananisha Kean wakiwa wawili tu kama ambavyo Kean alivo toa ahadi.
Mzee kasema hataki kumpigia simu na kumueleza deni hilo, kwa kuwa Kean alipo ahidi aliahidi kwa Mzee wake wakiwa uso kwa uso.
Hivyo kama Kean akimpigia simu Mzee wake basi wanaongea mambo mengine tu na suala la deni hilo huwa analinyamazia.
Kean wakati anakuwa na kujiunga na timu ya vijana ya Juventus alimuahidi kitu Mzee wake.
Kitu ambacho kinamuumiza kichwa hadi hii leo kwa kuwa bado hajakitimiza.
Kwa kauli iliotoka kinywani mwa Kean pasipo kushinikizwa na Mtu alimuahidi Baba yake kuwa kama siku akimuona ameanza kucheza Mpira klabuni Juventus na kuonekana kwenye Luninga basi atamnunulia Baba yake huyo trekta kwa ajili ya kilimo.
Mzee wake alifurahi mno baada ya kusikia kauli hio.
Na ukizingatia Mzee wake ana heka nyingi za Mpunga basi alijuwa ameukata.
Lakini hali ni tofauti.
Mpaka hii leo Mzee hajanunuliwa trekta wala hajatumiwa pesa kwa ajili ya kununua trekta.
Mzee alining’unika moyoni wee lakini sasa ameamua kulizungumzia.
Siku Juve walipotaka kumpa mkataba kamili Kean Mzee aliweka kipengele hicho kuwa mwanawe hawezi sajiliwa na Juve mpaka amnunulie trekta, lakini mwanasheria wa Juventus alikuwa mjanja na kumwambia kijana wake bado hajaonekana kwenye Luninga hivyo suala la trekta ni la kuli
0 comments:
Post a Comment