Friday, November 30, 2018

Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limeinyang'anya uenyeji wa AFCON 2019 nchi ya Cameroon baada ya kutoridhishwa na maandalizi waliyoyafanya.

Katika mkutano mkuu unaoendelea jijini Acra Ghana, CAF imefikia uamuzi huo baada ya kutolewa kwa ripoti mbili za uchunguz kutoka kamati ya usalama ya shirikisho hilo.

Ripoti ya kwanza ilikuwa na majibu ya ukaguzi uliofanywa kuanzia Otoba 27 hadi Novemba Mosi mwaka huu.

Ripoti ya pili ilikuwa na majibu ya ukaguzi uliofanywa kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 15.

Mwezi Oktoba, Rais wa CAF, Ahmad, alifanya ziara jijini Yaounde kukutana na  Rais wa Cameroon, Paul Biya, siku chache baada ya CAF ilipositisha mpango wa kufanya uamuzi wa mwisho kuhusu nchi ya kuandaa mashindano hayo.

Kufuatia uamuzi huo, CAF itatoa mwezi mmoja kwa nchi zinazotaka kupatiwa haki ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2019, kuwasilisha maombi yao.

Morocco, ambao waliomba kuandaa Kombe la Dunia la 2026, wanapewa nafasi kubwa kuchukua  nafasi ya Cameroon licha ya kuwa Afrika Kusini, wanatazamiwa kuipata nafasi hiyo.

Hii itakuwa mara ya pili kwa CAF kufanya maamuzi ya namna hiyo nchi uenyeji tangu Septemba 2017, ambapo Kenya ilipokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN) na nafasi yake kupewa Morocco.

Hata hivyo, mwaka 1995, Kenya kwa mara ya kwanza, walipokwa nafasi ya kuandaa AFCON 1996 kutokana na sababu za maandalizi hafifu na Afrika Kusini wakachukua nafasi hiyo.

0 comments:

Post a Comment