BONDIA Floyd Mayweather atapambana na kickboxer Tenshin Nasukawa huko Japan tarehe 31 Desemba, baada ya kusaini mkataba na kampuni ya sanaa ya martial arts.
BONDIA Huyo wa zamani wa uzito wa dunia Mayweather alishinda Conor McGregor wa UFC katika mechi iliyopigwa mnamo Agosti 2017 Na kuongeza rekodi yake kufikisha ushindi wa mapambano 50.
Hivi karibuni Mayweather amezungumzia mapambano Na Khabib Nurmagomedov wa UFC na Manny Pacquiao.
Sheria zitakazotumika katika mpambano huo na Nasukawa bado hazijatangazwa. "Nilitaka kufanya kitu tofauti," alisema bondia huyo mwenye umri wa miaka 41. "Nilitaka kuonyesha ujuzi wangu nje ya Marekani na kuwa Na mpambano maalum. Nataka kuwapa watu kile wanachotaka - damu, jasho na machozi."
Mayweather alisema sheria zitakazotumika katika mpambano huo zitajadiliwa "ndani ya wiki kadhaa zijazo". Nasukawa wa Japan, mwenye umri wa miaka 20, ana makubaliano na Shirikisho linalosimamia mapambano la RIZIN.
“Ilikuwa ni kutoa mshangao lakini nilikubali bila kusita," alisema Nasukawa, ambaye ana rekodi ya 27-0 katika kickboxing na rekodi 4-0 katika MMA.
"Ni wakati mkubwa zaidi katika maisha yangu na nataka kuwa mtu atakayebadilisha historia. Nitafanya hivyo kwa ngumi hizi, kwa pigo moja tu."
0 comments:
Post a Comment