Sunday, November 11, 2018

-Thierry Henry hapo jana ameendelea Kupokea kipigo akiwa kama kocha mkuu wa Monaco wamekutana na kipigo cha Magoli 4-0 wakiwa nyumbani Dhidi ya PSG.

PSG Sasa wanatimiza ushindi wa mechi nane dhidi ya Monaco Katika Mashindano yote..

Monaco msimu huu ni mbovu na haikuwahi kutoka kabla na Mara ya Mwisho ilikuwa ni August 1986 Ambapo hawakushinda Mechi 13 za Ligue 1, Msimu huu pia hajawashinda mechi yeyote Katika mechi 12 zilizopita za Ligue 1 (D4 L8)..

Vilabu  13 kati ya vilabu 14 ambavyo viliwahi kukusanya pointi 7 au ndogo zaidi ya hapo katika mechi 13 za mwanzo wa msimu wa Ligue 1 Katika karne ya 21 vilishuka  Daraja Mwisho wa msimu, Timu Pekee ikiyopona ni moja na mwisho wa msimu ilimaliza nafasi ya 16 ni  Ajaccio msimu wa 2011-12.

Edinson Cavani ni Mchezaji wa kwanza wa PSG kufunga Magoli 3+ Katika mechi Dhidi ya Monaco Ndani ya Ligue 1 tokea Carlos Bianchi ilikuwa ni May 25, 1979.

0 comments:

Post a Comment