NAHODHA MUONGOZA NJIA MAJINI:
Matthijs De Light ni moja kati ya mabeki bora kinda kwa sasa barani ulaya waliobahatika kuonekana na kupendwa sana. Amezaliwa mwaka 1999 , anamiaka 19 kwa sasa.
Alijiunga na Ajax akiwa na miaka 9 tu. Amechaguliwa kuwa nahodha wa Ajax kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa licha umri kuwa mdogo.
Kipindi Ajax inafuzu kwa mara ya mwisho kucheza nusu fainali ya Uefa Champions League alikuwa bado hajazaliwa ilikuwa mwaka 1997.
Lakini miaka 22 mbele Ajax inafuzu tena kwa kuwatoa vigogo Real madrid jatua ya 16 bora, wanakutana na Juventus Robo fainali wanawatoa.
Goli la ushindi linawekwa kimyani na kinda De Light hakika anastahili pongezi sana. Anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo mholanzi kufunga goli katika michuano ya Uefa champions league Tangu afanye hivyo Nordin wooter mwaka 1996.
0 comments:
Post a Comment