Manchester city imeibuka na ushindi wa goli mbili kw sifuri hii leo dhidi ya mahasimu wa manchester united katika dimba la Old Trafford. Magoli yamefungwa na Bernado sliva pamoja na Sane.
Kwa ushindi huo Pep Guardiola anakuwa kocha wa kwanza kushinda mechi tatu mfululizo akiwa ugenini dhidi ya manchester united.
Kikosi chake cha Manchester City leo kimeweka rekodi ya kufunga magoli mengi zaidi kuliko timu yoyote katika historia nchini Uingereza kwa msimu moja.
Kwa msimu huu pekee kwenye mashindano yote wamefunga jumla ya magoli 157.
0 comments:
Post a Comment