Wednesday, April 24, 2019

Young African Sports Club ,ilianzishwa  February 11.1935 ,ni zaidi ya miaka 84 imepita toka Club pendwa ya wananchi kinara wa kuchukua ubingwa ligi kuu  mara 27  ilipoanzishwa.

Tanzania,ikiwa na idadi ya jumla ya mikoa 31 na Wilaya zake 196 ,na jumla ya vyuo vikuu 71 Tanzania bara na visiwani ni  wakati sahihi wa Yanga African Sports Club kutengeneza ,"Club Ambassador, " kila chuo kikuu na kila Wilaya.

Ni wakati wetu kuitengeneza Yanga ,katika mfumo thabiti wa uwazi na uwajibikaji  katika kuwashirikisha wawekezaji wakubwa ambao ndio mashabiki.

Ukweli ulio uchi bila nguo,Yanga African ,ndio timu yenye mashabiki wengi Tanzania kuliko timu yeyeote ile ,sasa ni wakati sahihi wa kila mashabiki wa Yanga ,kuwekeza mahaba na mapenzi kwa timu pendwa katika kutoa support ili tuweze kuitawala ligi ya Tanzania bara tunavyotaka.

Tutakuwa na mfumo wa kuchukua wanafunzi bora darasani katika nafasi 10 ,ambao ni mashabiki wa Yanga na kuwapa nafasi ya kupiga picha na wachezaji wao wanaowapenda.

Ni muda sahihi wa kufanya mataendo ambayo yatuwezesha kuipeleka Yanga kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam Stock Exchange [DSE] na kuanza kupigania kufanya vyema kwenye soko la kimataifa.

Yanga ni dhehebu na mashabiki ndio waumini wa hili dhehebu bora lenye harufu ya ubingwa unao tamalaki Jangwani.

Yanga :Daima mbele nyuma Mwiko.

0 comments:

Post a Comment