Wednesday, December 27, 2017

Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante anamaliza mwaka 2017 kwa mafanikio makubwa baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ufaransa.

Kante amempiku nyota wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe kwenye tuzo hiyo.

Kante mwenye umri wa miaka 26 amepokea 'kijiti ' hiko cha tuzo kutoka kwa Antoine Griezmann ambaye alitwaa mwaka jana na kumzidi Mbappe kwa kura tano huku Straika wa Real Madrid, Karim Benzema akimaliza namba tatu.

Kante ambaye aliisaidia Leicester misimu miwili iliyopita kutwaa taji la ligi kuu ya soka ya Uingereza, aliisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu ya uingereza msimu uliopita.

Ubora wake ndani ya Chelsea ulimuwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Uingereza. Na pia kumaliza nafasi ya 8 katika tuzo za Ballon D'or 2017.

0 comments:

Post a Comment