Bosi wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amedai kuwa Daley Blind anapaswa kufikiria kuondoka Old Trafford kwenda Barcelona
Daley Blind amekosa nafasi kikosi cha kwanza kwenye timu ya Jose Mourinho kwani ameshindwa kucheza Ligi Kuu Uingereza tangu Septemba 23.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi amebakiwa na miezi sita tu kwenye mkataba wake, na Van Gaal ambaye alimsajili Blind 2014 - anaamini mchezaji huyo atafanikiwa Camp Nou ikiwa atajiunga na miamba ya Catalan kama wataipata saini yake.
Mdachi huyo alinukuliwa na The Mirror akisema: "Daley Blind ni bora aende Barcelona kuliko kubaki Man United. Hajakaa hata benchi United kwa muda. Daley anaweza kucheza kwenye nafasi zaidi ya moja na akienda Barcelona hatakalishwa benchi.
"Nadhani Daley ataifaa zaidi Barcelona. Kiwango chake na aina yake ya uchezaji inaendana zaidi na soka la Hispania kuliko Uingereza.
"Anaweza kucheza kama beki wa kati ambaye anaujenga mchezo. Anaweza kuwa kiungo mkabaji au beki wa kushoto mshambuliaji. Daley anaweza yote."
Kama inavyoonekana, Blind anaweza kuanza mazungumzo na klabu zinazovutiwa naye Januari.
0 comments:
Post a Comment