Manchester City wanaelekea Anfield jioni ya leo kuumana na Liverpool, Anfield ni uwanja ambao City amekuwa akipata matokeo mabovu mara nyingi, tangu 2003 hajashinda mchezo wowote katika dimba hilo. :
Liverpool watamakaribisha mfungaji bora wao Mohamed Salah, ambaye alikosa michezo miwili kutokana na majeruhi.
Nathaniel Clyne, Jordan Henderson, Alberto Moreno na Daniel Sturridge wote hawatocheza kutokana na majeruhi.
Manchester City kwa upande bado watamkosa Gabriel Jesus na mlinzi Vincent Kompany pamoja na Benjamin Mendy.
Takwimu
•Manchester City hawajapata ushindi Anfield tangu mwaka 2003, mechi 16 wameshacheza hapo tangu wakati huo katika mashindano yote. .
•Mara ya mwisho kwa Manchester City kuifunga Liverpool nyumbani na ugenini kwenye ligi ilikuwa msimu wa 1936-37, msimu ambao City wakishinda ubingwa wa ligi kwa mara ya kwanza. .
•Ushindi wa City wa 5-0 waliopata dhidi ya Liverpool katika raundi ya kwanza ya ligi, ndio ilikuwa mara ya kwanza kwao kufunga magoli 5 vs Liverpool tangu mwaka 1937.
:
Wakati City akiwa na mfululizo wa kushinda, Liverpool wao hawajapoteza mchezo hata mmoja katika mechi 17 zilizopita katika mashindano yote - mara ya mwisho kufungwa ilikuwa 22 October.
Endapo City watashindwa kupata ushindi, Liverpool watakuwa wamecheza mechi 12 za ligi za nyumbani bila kufungwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2011-12.
:
Endapo City watashinda leo, watakuwa klabu ya kwanza kushinda ugenini vs Manchester United, Chelsea na Liverpool ndani ya msimu mmoja wa ligi tangu Wimbledon walipofanya hivyo msimu wa 1986-87.
0 comments:
Post a Comment