Jose Mourinho amewaomba mashabiki wa Manchester United kuwa na uvumilivu katika hotuba ya dakika 12.
Mashabiki wa Manchester United walikasirishwa na kitendo cha Man United kuondolewa katika mashindano ya UEFA raundi ya 16 dhidi ya Sevilla siku ya Jumanne.
Mourinho kwa haraka sasa aliwakumbusha mashabiki hali aliyoikuta klabu hiyo na kusisitiza kwamba ataacha mradi mzuri sana kwa mrithi wake pindi akiondoka Old Trafford. " Sitokimbia, wala kupotea , wala kulia kwasababu eti nimezomewa na mashabiki, sitopotea katika korido ya kuingilia uwanjani, mechi ijayo nitakuwa wa kwanza kuingia uwanjani, siogopi majukumu yangu."
"Katika miaka saba iliyopita nafasi mbaya ya Manchester City ilikuwa namba nne , katika miaka saba iliyopita Manchester City walikuwa mabingwa mara mbili, ukitaka unaweza kusema pia mara tatu, walikuwa namba mbili mara mbili."
" Huo ni urithi . Unajua urithi ni nini ? Ni Nicolas Otamendi, Kevin De Bruyne, Fernandinho, David Silva, Raheem Sterling, Sergio Aguero, ni uwekezaji kutoka zamani, sio wa miaka miwili iliyopita. Unajua ni wachezaji wangapi wa Man United wameondoka klabuni msimu uliopita ? kuona wapi wanacheza, wanachezaje , kama wanacheza .? "
" Huo ni urithi wa soka. Siku moja nikiondoka, Kocha ajaye wa Manchester United atawakuta hapa Romelu Lukaku, Nemanja Matic na bila shaka David De Gea wa miaka mingi sana klabuni, atakuta wachezaji wenye uimara wa kiakili tofauti, wenye ubora, wakiwa na sifa tofauti na Ujuzi." Mourinho aliongeza : " Kwasababu fulani unaenda kwenye UEFA hatua ya robo fainali kama leo na kuna vilabu vinne ambavyo kila siku vipo hiyo hatua.
Barcelona huwa wanakuwa hatua hiyo katika miaka saba , nane iliyopita, Real Madrid , Bayern Munich, Juventus, na ndio kuna vilabu huwa vinakuja mara moja moja kama Inter Milan yangu, Monaco msimu uliopita lakini wale ambao mara zote wanafika hiyo hatua kuna sababu zake ."
" Kitu kizuri kwangu na hisia nzuri kwangu nipo katika ukurasa mmoja na wamiliki, Mr [Ed] Woodward, Mr [Richard] Arnold tupo katika ukurasa mmoja, tunakubaliana katika kila kitu, katika uwekezaji, ambao tunao na ule ambao tutaufanya msimu hadi msimu ,
Sunday, March 18, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment