Sunday, March 18, 2018

 Baada ya kusambaa kwa skendo ya kudaiwa kuchoropoa mimba takriban nane, muuza nyago maarufu Bongo, Tunda Sabasita amezungumza na Risasi Jumamosi na kuanika ukweli wa mambo.

Mrembo huyo ambaye amekuwa gumzo siku za hivi karibuni kutokana na kudaiwa kuwa na msururu wa wanaume, ameibuliwa skendo hiyo ya kuchoropoa mimba baada ya kusambaa kwa picha yake mpya inayomuonesha kama ni mjamzito.

ETI NI NDANI YA MIAKA MICHACHE TU

Madai hayo mazito yaliyoporomoshwa mtandaoni, mbali na kutaja idadi hiyo ya kutisha, yalizidi kumtafuna mrembo huyo kwa kudai amefanya matukio hayo yote ndani ya miaka michache iliyopita.

HUYU HAPA TUNDA

Akizungumza na Risasi Jumamosi katika mahojiano hayo maalum, Tunda alisema anashangazwa na madai hayo kwa sababu katika hali ya kawaida mtu huwezi kuchoropoa idadi hiyo ya mimba na bado ukaendelea kufanya shughuli zako kama kawaida.

Alisema katika hali ya kawaida, si rahisi kabisa kwani kama kweli angefanya hivyo, lazima angepata madhara na hata afya yake ingezorota. “Jamani kweli mtu unaweza kuchoropoa mimba nane tena ndani ya kipindi kifupi? Sidhani kama unaweza ukawa binadamu sahihi kabisa na binafsi sijawahi kutoa mimba kama watu wanavyodai,” alisema Tunda.

huyo aliendelea kusema kuwa watu wanaweza kumsema hivyo kutokana na tumbo lake lilivyo kwani mara nyingi akifanya mazoezi linapungua, akiacha linakuwa kubwa na watu kudhani ana mimba.

 “Hili tumbo wanaweza kulishangaa lakini ni kwamba liko hivyo siku zote kama sijafanya mazoezi muda mrefu na pia sijinyimi kwenye kula chakula kabisa, linakuwa kubwa utadhani nina mimba kumbe walaa,” alisema Tunda ambaye ameuza nyago kwenye video ya Wimbo wa Why Me ya Amini Mwinyimkuu na Elias Barnaba.

Tunda aliongeza kuwa, watu wengi wanamtabiria ana ujauzito kitu ambacho sio kweli kwani hajawahi kushika mimba hata ya kusingiziwa.

“Mimi napenda tu watu wafahamu kuwa sijawahi kushika mimba ya mtu yeyote kama wanavyosema siku zote na wala sijawahi kutoa maana tumbo langu ndivyo lilivyo,” alisema Tunda.

0 comments:

Post a Comment