Wednesday, May 30, 2018

Aston Villa wamethibitisha kwamba John Terry  ataondoka klabuni hapo pindi mkataba wake utakapofikia tamati mwezi ujao.

Terry, 37, alijiunga na Villa kwa mkataba wa mwaka mmoja majira ya kiangazi yaliyopita baada ya kuondoka Chelsea na kufanikiwa kufunga goli moja katika mechi 36.

Hata hivyo Villa walishindwa kupata nafasi ya kurejea kucheza ligi kuu ya Uingereza baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Fulham siku ya Jumamosi.

0 comments:

Post a Comment