Baada ya kiungo wa AS Roma Radja Nainggolan kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubeligiji kitakacho safiri kwenda Urusi kwenye fainali za kombe la Dunia, kocha wa timu ya taifa Roberto Martinez ametoa sababu za kumuacha.
" Radja Nainggolan ni mchezaji wa daraja la juu, sababu za kumuacha ni za kiufundi."
" Katika miaka miwili iliyopita timu ilikuwa inafanya kazi kwa staili fulani , wachezaji wengine walikuwa na majukumu mengine."
" Tunajua Radja ana majukumu muhimu katika klabu yake na hatuwezi kumpa hilo jukumu katika kikosi chetu."
0 comments:
Post a Comment