Maurizio Sarri ameashiria kwamba huenda akaondoka Napoli majira haya ya kiangazi kwa kusema kwamba " kila kitu kinafikia mwisho wake " baada ya kuhusishwa na Chelsea.
Muitaliano huyo alifanya mazungumzo na Rais wa klabu hiyo Aurelio De Laurentiis siku ya Jumatano kuhusu mustakabali wake , lakini Sarri amekiri kwamba bado hajafanya uamuzi kuhusu wapo atafundisha msimu ujao.
Amehusishwa sana na kuchukua nafasi ya Muitaliano mwenzake Antonio Conte ndani ya Chelsea ambaye mustakabali wake ndani ya Stamford Bridge upo shakani licha ya kutwaa taji la kombe la FA .
" Katika maisha kila kitu kina mwisho wake. Kuna muda ni vizuri kumaliza stori pindi zinapokuwa nzuri . Pindi nilipofika hii timu ilimaliza kwa tofauti ya Pointi 24 kutoka kileleni . Sasa hivi tupo pointi 4 nyuma . hatujafikia lengo lakini safari imekuwa nzuri . kesho nitaongea na familia yangu kabla ya mtu yoyote . Rais wa klabu anataka majibu haraka . Sidhani kama naweza kuhamia klabu nyingine ya Italia haraka hivyo . kumbukumbu ya Napoli ipo bado kichwani."
0 comments:
Post a Comment