Barcelona wapo tayari kuingia kwenye vita dhidi ya Arsenal na Chelsea katika kumuwania beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sport.
Koulibaly alikuwa na msimu mzuri sana ndani ya Napoli na anawindwa sana Barani Ulaya , huku Barcelona wakiandaa ofa ya kumnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 26.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania , jarida la Sport Barcelona wanajiandaa kutoa ofa ya Euro Milioni 40 pamoja na wachezaji watatu Andre Gomes, Denis Suarez na Paco Alcacer.
0 comments:
Post a Comment