Saturday, June 2, 2018

Kupitia ukurasa wake wa instagram mchambuzi wa soka nguli nchini tanzania amefunguku hivi

"Barthez amefungwa magoli yanayofanana na yele aliyowahi kufungwa enzi zake wakati yupo Yanga."

Ally Mustapha 'Barthez' ni mbovu wa mipira ya juu, kama utakumbuka goli la kona alilifungwa leo na Baba Ubaya ni kama goli ambalo alifungwa na Shiza Kichuya akiwa Yanga. Goli la kwanza alilofungwa na Salum Kihimbwa linafanana na ambalo aliwahi kufungwa na Okwi akiwa Yanga.

Barthez ni golikipa mwenye uwezo anashindwa kuhimili mipira ya juu kutokana na kimo chake (mfupi) ndiyo maana wenzetu walioendelea (Ulaya) wanatumia kanuni yao ya golikipa lazima awe mrefu, sio wajinga.

Ufupi wa Barthez umekuwa disadvantage kwa Singida United hususan mbele ya wachezaji wenye uwezo mzuri wa kupiga mipira juu.

Shaffih amesahau kipa wa leicester city ni mfupi lakini anafanya poa langoni ufupi siyo kikwazo ila ni mbinu za udakaji.

0 comments:

Post a Comment