Saturday, June 2, 2018

Mapacha wawili walioungana, Maria na Consolata wafariki dunia usiku huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakipatiwa matibabu

Tangu mwishoni mwa mwaka jana, mapacha hao walifanyiwa uchunguzi mara kadhaa baada ya kupata matatizo ya moyo

Katika jitihada za kutafuta suluhu ya ugonjwa wao, walifika kupatiwa matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam

Katika safari ya elimu, Maria na Consolata walionesha uwezo mkubwa tangu walipohitimu na kufaulu Darasa la Saba mwaka 2010 katika Shule ya Msingi ya Ikonda wilayani Makete

Baadaye walijiunga na Kidato cha Nne katika shule ya Sekondari ya Udzungwa iliyopo Wilayani Kilolo

Walisoma pia kidato cha 5 na 6 katika shule hiyo na baadaye walijiunga na Elimu ya Juu katika Chuo Kikuu cha Ruaha(RUCU) baada ya kupata daraja la 2 katika mtihani wa Kidato cha 6

Maria na Consolata walizaliwa katika Hospitali ya Misheni ya Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe mwaka 1996.

0 comments:

Post a Comment