Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa upo kwenye mazungumzo na mchezaji Mzambia, Obrey Chirwa, kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu yao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema kuwa wameanza mazungumzo naye kuona kama wataweza kuongeza naye mkataba mwingine.
Nyika ameeleza Chirwa ameshamaliza mkataba na Yanga baada ya muda wake wa miaka miwili kuisha tangu asaini mwaka 2016 akitokea FC Platnumz ya Zimbambwe.
Wakati Yanga wakianza mazungumzo naye, watani zao wa jadi, Simba, wanaelezwa kuingia katika rada za kumuwania mchezaji huyo ambaye amekuwa amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu kuhitajika kwa wekundu wa Msimbazi.
Mbali na Simba, klabu kadhaa nje ya Tanzania ikiwemo Ismailia ya Uarabuni nayo imeelezwa kuwania saini ya mchezaji huyo ambaye alikuwa mmoja ya waliokuwa tegemo ndani ya kikosi cha Yanga.
0 comments:
Post a Comment