Monday, July 30, 2018

Everton watakamilisha usajili wa beki wa kushoto kutoka Barcelona  Lucas Digne katika saa 24 zijazo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikuwa na Barcelona katika maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani , lakini mabingwa wa La Liga wamethibitisha kwamba Digne amerejea Hispania kukamilisha uhamisho wa kutua Everton .

Barcelona waliandika hivi kupitia ukurasa wao rasmi wa Twitter .

" Lucas Digne amesafiri leo ( jana jumapili ) kwenda Barcelona kwa ruhusa ya klabu kukamilisha uhamisho wake wa kuondoka klabuni."

Na Digne nae aliwashukuru Barcelona kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema," Nataka kuwashukuru wote kwa kusema asante . kwanza kabisa kwa klabu ambayo imenipa kila kitu tangu nilipofika."

0 comments:

Post a Comment