Wednesday, July 25, 2018

Nadhani klabu ya Barcelona ni moja ya timu ambayo kocha apati shida  kubwa kwenye kupanga kikosi kutoka na ule muanganiko miongoni mwa wachezaji (players chemistry ).

Tunaona upande wa nyuma kina Samwel Umtiti ,Gerald Pique kupamudu vizuri ,Upande wa kiungo wa kukaba (Holding mildfielder ) Kwa mfumo ambao Barcelona wanatumia kwa takribani misimu sita Busquet ameimudu hiyo nafasi .

Miaka takribani 10 Sasa A.Iniesta ndio alikuwa anacheza nafasi ya kiungo  Mshambuliaji kwa maana ya namba 8 kwa mfumo wa kiswahili ambao ukipa timu Jamhuri Kiwelu au Felix Minziro atakwambia kiungo mwenye jicho la tatu.

Msimu mpya wa la liga unaanza kwa kuwakosa kuwaona Ronaldo ,Iniesta,Torres,na Gabi ambao wameviama vilabu vyao.

Upande wa Barcelona umeingiza maingizo mapya kwa maana Malcom ameingia kwenye timu,maana Countiho atachukua Kazi ya iliyoachwa na Iniesta huku Suarez na Mr captain Leonel Messi wakiwa sehemu ya ufungaji.. Swali ni
Osmane Dembele au Malcolm ?

Upande wa winga Barcelona inawachezaji wawili ambao wanafanana uchezaji ,Je nani anastahili kuanza kati ya Osmane na Malcom.
Hizii  ndio takwimu zao kwenye soka la ngazi ya klabu.

Dembele
MICHEZO 102
Pasi za msaada wa mabao 35
Magoli 26.

Malcom
MICHEZO 150
Magoli 30
Pasi za msaada wa mabao 21.

0 comments:

Post a Comment