Wednesday, July 25, 2018

Staa wa Pop, Rock na Rnb Demi Lovato amekata kuwapa taarifa madaktari kuhusu dawa gani alitumia kwa kupitiliza iliyopelekea kuwa OverDose mpaka kupelekwa hospitalini.

Taarifa ilitolewa na TMZ kuhusu Overdose ya staa Demi Lovato iliyopelekea kupatiwa huduma ya kwanza nyumbani na kupelekwa hospitalini.

Polisi walihisi ni Heroin ila marafiki wa Demi walikanusha taarifa hizo huku mgonjwa akikataa kusema ni dawa gani alitumia kitu ambacho kitazuia polisi kufungua mashtaka dhidi yake na matumizi ya dawa za kulevya.

Demi alipewa dawa ya Narcan ambayo huzuia Overdose ya dawa za kulevya. Fahamu Lovato ana historia ya matumizi ya cocaine na Oxycontin ila amekuwa msafi kwa muda wa miaka 6.

Polisi wanasema hakuna kesi dhidi yake sababu hawakupata dawa hizo nyumbani kwake na hakuwa nazo kwenye mwili wake.

0 comments:

Post a Comment