Tuesday, September 18, 2018


Mbali na kutoa tiketi 250 za VIP bure, Mkurugenzi wa Masoko wa Azam TV Abdul Mohamed pia ametangaza ofa nyingine kwa wenye ving'amuzi vyenye matatizo.
Amesema "Kama una king’amuzi kibovu kilete, na Azam TV itakupa king’amuzi kingine, kwa sharti moja la kulipia kifurushi chako cha Pure kwa miezi minne. Pia kama rimoti yako inasumbua, ilete tutakupa mpya kwa sharti la kulipia kifurushi chako cha pure kwa miezi miwili.

Meneja wa Michezo wa Azam Media Baruan Muhuza amesisitiza kuwa matangazo ya mechi hiyo kati ya Simba na Yanga yatakuwa na ubora wa hali ya juu na yataondoa kila aina ya utata unaoweza kuwepo kama ambavyo imeonekana kwenye mechi za msimu huu
Msemaji wa Yanga Dismas Ten amekiri kuwa Simba ni timu bora tangu msimu uliopita hadi sasa, na ina wachezaji wazuri zaidi lakini na wao wamejiandaa kiutofauti kuwakabili siku hiyo ya Jumamosi Septemba 30, 2018 akisema
“Maandalizi ya mechi kama hii ni tofauti na maandalizi ya mechi nyingine.

0 comments:

Post a Comment