Thursday, September 20, 2018

Jana mlinda lango Klaus Kindoki alipooneka kuanza kwa mara ya pili licha ya kufanya vibaya kwenye mchezo uliopita, wengi walikosoa uamuzi huo wa kocha Mwinyi Zahera bila kuelewa.

Ukweli ni kwamba kwenye mchezo dhidi ya Stand Kindoki alifanya makosa ya kimchezo na kumuanzisha jana ilikuwa ni lazima ili kumjenga kisaikolojia na kutomuondolea kujiamini licha ya lawama kutoka kwa mashabiki.

Kindoki ni mmoja wa walinda lango bora sana na hakuna shaka hilo atalidhihirisha kadiri atakavyopata nafasi ya kukaa langoni.

Wakati mwingine ni vyema kuwaamini wachezaji na kuwapa nafasi nyingine pale wanapofanya makosa kwani na wao ni binadamu.

Mpira ni mchezo wa makosa na kama mwanadamu siyo kila siku utakuwa mkamilifu. Mpira unahitaji uzoefu ili kuumudu vizuri, kindoki anahitaji mechi nyingi ili kuwa vizuri na kuelewana na mabeki hasa nahodha kelvin yondani pamoja na vincent andrew.

0 comments:

Post a Comment