Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Simba Mtemi Ramadhani ameamua kujiondoka katika kinyang'anyiro hicho.
Mtemi Ramadhani ameweka bayana sababu zilizomfanya aondoe jina lake kugombea uenyekiti wa klabu ya Simba huku uchaguzi ukiwa umepangwa kufanyika mwezi unao.
"Ni kweli nimeandika barua kwenda kwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba kwamba naomba jina langu liondolewe kwenye kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba."
"Sababu kubwa sasa hivi nina majukumu mengi ninaweza kuhamia Dodoma kwa hiyo nadhani sitaweza kuitumikia vyema klabu yangu ya Simba lakini pia ningependa kuona klabu ina umoja katika kipindi hiki ambacho tunataraji kutetea ubingwa wetu ambao tuliupata msimu uliopita."
"Mara nyingi hizi chaguzi zimekuwa zikiwagawa wanachama, kipindi hiki tunahitaji umoja hiyo ni sababu nyingine imenifanya nifikirie kuacha kugombea nafasi hii."
"Nafasi hizi za kuhudumia watu ni ngumu, watu huwa hawazikimbilii kwa hiyo nimeona nitoe nafasi kwa mtu yeyote anayeweza kuongoza klabu ya Simba aweze kuogoza mpaka hapo tutakapofika."
"Katika kipindi hiki kuna mchakato wa kuitoa klabu kutoka sehemu moja kwenda nyingine, tunahitaji uongozi imara unaoweza kututoa hapa tulipo. Rai yangu kwa wanachama tuchague viongozi waadilifu na imara ambao watatusaidia."
Kujiondoa kwa Mtemi Ramadhani inamaanisha Sued Nkwabi anabaki pekeyake kugombea nafasi ya uenyekiti wa Simba kwa sababu kwa muda uliosalia hauruhusu mtu mwingine kuingia kugombea.
0 comments:
Post a Comment