Mwenyekiti kamati ya usajili yanga Hussein Nyika amekanusha vikali taarifa zinazozagaa mitandaoni kuwa kocha mkuu wa Yanga amemkataa obrey chirwa .
Hussein nyika amesema " mpaka chirwa anaondoka yanga alishaonana na viongozi na tulimpa baraka zote sasa amerudi nyumban nadhani hakuna kosa , hakuna asiejua uwezo wa chirwa uwanjani."
"Hakuna binadam aliekamilika na pia hakuna anaejua matatizo ya chirwa isipokuwa Sisi viongozi wa Yanga ".
"Kocha anajua uwezo wa chirwa uanjani na hajawahi kuwa na kinyongo na chirwa na Ana mkubali 100% chirwa si wa kufanyiwa majaribio mambo yakikamilika tutaweka hadharani kama suala la kocha kuhusu chirwa kocha amekubali na tupo hatua za mwisho kumalizana nae."
"Sasa nashangaa vyombo vya habari na magazeti pamoja na mitandao ya kijamii inavyomchafua kocha pamoja na chirwa naweza kusema huu sio uungwana kabisa."
"Si chirwa tu mbona hata katika vilabu vingine wachezaji huondoka na kurudi jamani sio dhambi cha msingi ni makubaliano tu ya pande mbili pamoja na bench la ufundi."
"Tusimsemee kocha vibaya wakati kocha anamkubali chirwa."
"Leo tunanamechi na KMC naomba mashabiki na wanachama tujitokekeze kwa wingi ili tutimize wajibu wetu na malengo tuliojiwekea kuhakikisha msimu huu tunarudisha ubingwa Jangwani. Yanga n klabu kubwa na kushinda ndio utamaduni wetu."
"Mwisho. Tutasajili mchezaji dirisha dogo kulingana na hitaji la kocha na bench la ufundi kwa UJUMLA na si mihemko ya watu wasiopenda maendeleo ya timu yetu. "
"Pia ushindi tunayoipata n kulingana na umoja na mshikamano wetu pamoja.
Msisahau kuichangia yanga . "
Nyika alimaliza kwa kusema kauli mbiu ya Yanga
"Daima MBELE nyuma mwako."
Together we can
We are one.
0 comments:
Post a Comment