Monday, November 19, 2018

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike amesema kuwa anaangalia kujituma kwa mchezaji katika mazoezi na sio kupanga tu ilimradi ana jina kubwa.

Amunike Amesema kuwa anapanga Kikosi Kwa kufuatia Mazoezi jinsi Mchezaji anavyojituma Kwa ajili ya timu.

"Tumefanya Mazoezi kwa siku kumi kule afrika kusini, nimepata muda wa kuwatathimini wachezaji wote, lakini siwezi kutoa maelezo ya ndani zaidi kuhusu wachezaji wetu, nawapanga wale walio tayari kujitoa kwa ajili ya timu, bahati mbaya wengine hawapo kwenye ubora wao, sio kwamba namkosoa mchezaji yoyote, hapana simkosoi john boco, wala sio mkude, hii sio Simba ni timu ya taifa, huu ndio ukweli.. Alisema kocha Amunike.

"najua kila mtu ana mchezaji wake kipenzi ambaye angependa kumuona akicheza, lakini Sisi tunaangalia mchezaji lakin sis tunaangalia mchezaji mmoja mmoja anavyojitoa kwenye mazoezi, na hicho ndicho tunachokitaka" Aliongeza kocha Amunike

0 comments:

Post a Comment