Tuesday, November 13, 2018

Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limethibisha mashindano ya Kombe la Chalenji 2018 Maarufu kama "CECAFA Challenge Cup" yaliyokuwa yaanze mwishoni mwa mwezi huu, hayatafanyika tena.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema wameshindwa kupata nchi iliyokuwa tayari kuwa mwenyeji wa fainali hizo baada ya Kenya kujitoa Kwa sababu ya ukata wa fedha za maandalizi ya michuano hiyo.

Kenya ilipata haki za kuwa mwenyeji wa mashindano hayo baada ya kuwa Bingwa Kwa msimu Uliopita wa Fainali hizo  kuifunga Zanzibar kwa penalti na kutwaa ubingwa huo mwaka jana... Hivyo Sasa Michuano hiyo inatarajia kufanyika tena Mwezi Julai ya Mwaka 2019, na kabla ya hapo yatafanyika Mashindano ya Kagame Cup Kwa Vilabu vya ukanda wa CECAFA yanayotarajia kuanza mapema mwezi Juni mwakani.

0 comments:

Post a Comment