Tuesday, November 13, 2018

Real Madrid wamethibitisha Santiago Solari  kuwa kocha wao mpya na kusaini mkataba wa miaka mitatu utakaofikia tamati mwaka 2021.

Awali iliripotiwa Solari atapewa timu mpaka mwishoni mwa msimu huu lakini Florentino Perez ameamua kumpa kiungo huyo wa zamani wa Real miaka mitatu ya mkataba.

Solari sasa anakuwa kocha wa tatu mfululizo ambaye amewahi kukipiga Santiago Bernabeu.

Zidane ⚽️👔
Lopetegui ⚽️👔
Solari ⚽️👔

0 comments:

Post a Comment