Friday, October 25, 2019

Kocha wa klabu ya soka ya Pyramids fc, Sébastien Desabre amesema hana hofu na uwanja kubadilishwa kwa kua wachezaji wake ni ‘ proffesionals ‘ hivyo ni lazima wajue kubadilika kulingana na mazingira.
.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa, aliongeza kua timu yake inawachezaji ambao wamecheza michuano ya kimataifa kwa muda mrefu na wamepita viwanja mbalimbali hivyo itakua rahisi kuendana nao.
.
AIGUSIA YANGA, AMTAJA JUMA BALINYA..
.
Pia Desabre ameongeza kwamba anaifahamu yang
a kwakua ameishi Afrika Mashariki kwa muda hivyo atajaribu kufaidika na ufahamu huo.
.
“Nimekaa Afrika mashariki, naifahamu Yanga na baadhi ya wachezaji kama Balinya, hivyo nitajaribu kuifanya timu ifaidike na uzoefu mdogo nilionao kuhusu timu za ukanda huu.” - aliongeza Desabre ambaye pia amewahi kufundisha Wydad Ac, Ismaily pamoja na timu ya taifa ya Uganda kabla ya kutua Pyramids fc.

0 comments:

Post a Comment