Tuesday, October 15, 2019

Uhuru suleiman amefunguka mengi kuhusiana na mshambuliaji wa Yanga sc David Molinga Ndama "falcao" kutokana na maneno aliyo yasikia DRC Congo alipo kwa sasa.

"Baada ya mimi kutua DC Motema Pembe kila mchezaji alikuwa akimzungumzia Molinga ambaye huko anajulikana kwa jina na Falcao."

"Wanasema kuwa ni bonge la mshambuliaji, anajua sana kufunga, sema tu kabla ya kuja Yanga alikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita bila kucheza kutokana na kuwa majeruhi."

"
Kwa hiyo Yanga wampatie muda tu kwani kutokana na jinsi wanavyomzungumzia huko DR Congo naamini atawasaidia hata katika mchezo dhidi ya Pyramids anaweza kufanya vizuri kutokana na kuwa na uzoefu na mechi za kimataifa" - Uhuru Suleiman (Mshambuliaji DC Motema Pembe)

0 comments:

Post a Comment