Tuesday, November 12, 2019

mshambuliaji wa manchester city na timu ya taifa ya England raheem sterling ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kitakacho cheza dhidi montenegro alhamisi  mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020.

chama cha soka cha England ( FA )  kimethibitisha hilo na kutolea ufafanuzi sababu kuu ni kutokana na vurugu alizo mfanyia beki wa liverpool Joe Gomez wakati wa mazoeziya timu ya taifa ya England.

Sterling na Gomez ugomvi wao ulianza weekend iliyopita kwenye mchezo kati ya manchester city dhidi ya liverpool katika dimba la anfield mara baada ya Gomez kumsukuma Sterling na kuanza kutunishiana vifua mchezo huo uliisha kwa liverpool kuibuka na ushindi wa goli 3 - 1.

aidha uamuzi huo  wa kumsimamisha Sterling umechukuliwa na timu nzima ya england iliyo chini ya kocha mkuu southgate

0 comments:

Post a Comment