Thursday, December 28, 2017

               

Arsenal wamepeleka ofa ya Pauni Milioni 35 kwa Juventus kwa ajili ya kupata saini ya beki Medhi Benatia, kwa mujibu wa taarifa kutoka Italia.

Arsene Wenger yupo tayari kuimarisha kikosi chake mwezi Januari na tayari anataka kufanya maboresho katika safu yake ya ulinzi.

Sky Italia imearifu kwamba Gunners wamewasilisha ofa hiyo kwa ajili ya kumnasa Benatia ambaye alijiunga na Juventus kwa uhamisho wa kudumu kutoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu uliopita.

Lakini taarifa zinasema kwamba Juventus wamekataa ofa hiyo na hawapo tayari kumuuza beki huyo wa kimataifa wa Morocco.

0 comments:

Post a Comment