Waingereza na Kura zao.
Tovuti ya Sky Sports kuanzia wiki iliyopita waliomba mashabiki wa soka wa ligi kuu ya Uingereza kupiga kura kuchagua kikosi bora cha msimu huu mpaka sasa.
Wachezaji wa Manchester City wanatawala kikosi hiko wakitoa wachezaji wanne kati ya wachezaji 11 wa kikosi husika.
Kyle Walker, Nicolas Otamendi, Kevin De Bruyne na Raheem Sterling wote wapo ndani lakini David Silva amekosekana, akipoteza kwa kura 29 dhidi ya Philippe Coutinho kutoka Liverpool.
Na kikosi ambacho kinaonekana cha kushambulia zaidi , lakini chaguo lililokamata mitazamo ya watu ni lile la Golikipa wa Manchester United David De Gea ambaye alishind kwa kura 80, zaidi ya mchezaji mwingine yoyote yule.
Na hiki ndio kikosi kamili:
GK: David de Gea
RB: Kyle Walker
CB: Cesar Azpilicueta
CB: Nicolas Otamendi
LB: Marcos Alonso
CM: Eden Hazard
CM: Philippe Coutinho
CM: Kevin De Bruyne
RW: Raheem Sterling
LW: Mo Salah
ST: Harry Kane
0 comments:
Post a Comment