suarez awakarbisha countinho na griezmann
Luis Suarez amesema kwamba atawakaribisha wachezaji wapya Antoine Griezmann na Philippe Coutinho ndani ya dimba la Camp Nou.
Vinara hao wa La Liga wamekuwa wakihusishwa na usajili wa fedha nyingi kwa nyota wa Atletico Griezmann na kiungo wa Liverpool Coutinho.
Suarez amewasifia wachezaji wote wawili na kusema kwamba wote wanatafiti vizuri kweny kikosi cha Barca.
Akiongea na Jarida la Echo, Suarez amesema," Wote wawili Griezmann na Coutinho ni wachezaji wa daraja la juu sana . Wote wawili bado ni wadogo na wana maisha marefu sana katika soka lao . Siku zote Barca wanapenda wachezaji bora." Suarez pia amesema kwamba ataweza kucheza sambamba na Griezmann katika kikosi kimoja , tofauti na wazo kwamba Mfaransa huyo atakuja kucheza badala yake.
Ameongeza," [Griezmann] sio namba 9. Atletico pale anacheza na straika mwingine pamoja . Ni wazi kwamba Griezmann atakuja kuisaidia timu katika nafasi ambayo kocha atataka ." #sokaliveupdates
0 comments:
Post a Comment