Monday, December 18, 2017

Kupitia mtandao wa instagram vanessa mdee ambaye ni mwana mziki wa kike anaye fanya vizuri kwa sasa nje na ndani ya tanzania amethibitisha kusaini mkhataba na lebo ya kimataifa universal.

Na sasa anaungana na diamond platinum kuwa chini ya label hiyo.

Vanessa aliandika hivi "Kama ilivyo ada, tunaanza kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa baraka zake na kibali chake cha kutufikisha siku njema ya leo."

"Nawashukuru mashabiki wangu, ndg, jamaa na marafiki wa karibu, tuliokuwa sambamba tangu mwaka unaanza mpaka hivi sasa tukielekea ukingoni."

"Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu;
Mwanzoni mwa mwaka huu,
Nilipitia changamoto nyingi Sana
Lakini kwa neema za Mungu , Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu."

"Ikiwemo kuwa mmoja wa familia ya  Universal Music Group in a unique joint signing between universalmusicgermany airforce1 na universalmusicgroup  na hii ni mara ya kwanza kwa Msani wa Kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuuuuuuuuuuu sana"

"Hii ni habari njema kwa mashabiki wangu na ndiyo kwanza tumeanza. Mambo makubwa zaidi yanakuja . Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndiyo mwanzo wa jumatatu"

0 comments:

Post a Comment