Kikosi cha Yanga jana kilirejea mazoezini baada ya mapumziko ya siku moja kufuatia mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ndanda uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mazoezi hayo yalifanyika chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam na yalisimamiwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera.
Hata hivyo Zahera anatarajiwa kuondoka wakati wowote kwenda kwao DR Congo kutimiza majukumu ya kikosi cha timu ya Taifa.
Kocha Msaidizi Noel Mwandila anatarajiwa kuachiwa majukumu ya kuinoa Yanga mpaka hapo Zahera atakaporudi baada ya Novemba 18.
Katika mazoezi hayo Yanga imeendelea kumkosa kiungo wake Mcongo Papi Tshishimbi ambaye amerejea kwenye orodha ya wachezaji majeruhi baada ya kutonesha goti.
Juma Mahadhi na Baruani Akilimali wameendelea kuwa nje kutokana na majeruhi ya muda mrefu.
Yanga pia inajifua bila wachezaji wake wanne Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Feisal Salum walio kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichoweka kambi nchini Afrika Kusini.
Ramadhani Kabwili, Abdallah Shaibu na Godfrey Paulo 'Boxer' nao wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya vijana U23.
0 comments:
Post a Comment