Wednesday, June 6, 2018

Klabu ya Manchester United imethibitisha rasmi kukamilisha usajili kwa beki wa pembeni Diogo Dalot kutoka katika klabu ya FC Porto kwa mkataba wa miaka mitano kukiwa na kipengele ya kuongezea mwaka mmoja.

Dalot ambaye anaichezea timu ya taifa ya Ureno chini ya miaka 21, amesajiliwa kwa kiasi cha Pauni Milioni £19m huku akiwa na uwezo wa kucheza kama beki namba tatu na namba mbili.

0 comments:

Post a Comment