Bayern Munich wanajiandaa kufanya mazungumzo na klabu ya RB Leipzig ili kupata saini ya straika wao Timo Werner, kwa mujibu wa taarifa kutoka Bild.
Huku kukiwa na mashaka kuhusu hatima ya Robert Lewandowski , mabingwa hao wa Bundesliga wanajiandaa maisha bila ya nyota huyo wa Poland na sasa wamemuona Werner kwamba ni Straika sahihi kumrithi Lewandowski.
Hata hivyo inaonekana ada ndio itakuwa kikwazo kikubwa kwasababu Leipzig wameripotiwa kuhitaji Pauni Milioni 100 kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 22.
0 comments:
Post a Comment