Sunday, June 3, 2018

Ni majuzi tu mkemi ametoka kuzikanusha habari za kujiuzuru lakini mara baada tu ya mkubwa kuvuliwa nguo leo ime mpasa kuchutama.

Yanga leo imeburuzwa nje kwenye michuano ya sportpesa supercup kwa kupigwa magoli ma tatu kwa moja dhidi ya kakamega home  boys.

Kupitia ukurasa wa instagram kiongozi mzito wa yanga imebidi achutame inamaana kajivua uongozi

Ameandika hivi  "Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi
Kwa Hakika Tumepata Aibu
Kubwa
Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili
Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza
Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.
Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club "YANGA " kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.
Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu
SALUM MKEMI
NIMENG'ATUKA"

0 comments:

Post a Comment