Wednesday, June 6, 2018

Antoine Griezmann amewaambia marafiki zake wa karibu kwamba atakataa ofa ya kuhamia Barcelona na kusaini mkataba mpya ndani ya Atletico Madrid , kwa mujibu wa taarifa kutoka Marca.

Barca walikuwa wanajiamini tayari wameshamnasa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa dau la Euro Milioni 100 lakini Griezmann anataka kulipa fadhila kwa Diego Simeone ambaye amemsaidia kumbadilisha na kuwa mmoja wa wechezaji bora Duniani.

Ubingwa wa Europa mwezi uliopita nao umeripotiwa kumshawishi Griezmann kwamba anaweza kutwaa mataji zaidi ndani ya Wanda Metropolitano.

Mkataba mpya wa Griezmann utapandisha thamani yake na kumfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa dau kubwa Duniani.

0 comments:

Post a Comment