Tuesday, June 5, 2018

Mbunge wa Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete amesema anaweza kufikiria kuwekeza katika klabu ya Yanga kama klabu hiyo itabadili mfumo wake wa uendeshaji.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya kikwete amenukuliwa na moja ya redio maarufu nchini akisema anaweza kushawishika kuwa mmoja wa wawekezaji katika klabu hiyo kama itabadili mfumo wake wa uendeshaji.

Ridhiwani amesema Yanga inahitaji mfumo sahihi wa uendeshaji wa mpira ambao utaweza kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za kukosekana kwa pesa ili waweze kufanya vizuri.

Baadhi ya wanachama wamekuwa wakimpigia 'chapuo' Ridhiwani agombee Uenyekiti wa Yanga kwenye Mkutano Mkuu utakaofanyika wiki ijayo, Juni 10, mwenyewe amekataa.

Wanachama wa klabu ya Yanga wanatarajia kutumia Mkutano Mkuu wa Jumapili ijayo, kubariki mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kama yalivyo kwenye Katiba ya timu hiyo.

0 comments:

Post a Comment