Tuesday, June 5, 2018

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Manchester United, Paul Pogba ameeleza kwa mara ya kwanza kuwa mahusiano yake kwa sasa na kocha Jose Mourinho hayupo sawa.

Pogba akihojiwa na mtandao wa French Football wikiendi iliyopita baada ya mechi ya Italia na Ufaransa amedai kuwa msimu mzima alikuwa na majeraha ndio maana amekuwa benchi muda mwingi lakini amekuwa na mkosi zaidi baada ya kuvurunda kwenye mchezo dhidi ya Newcastle United ambapo Man United walipigwa goli 1-0 .

“Mimi sio kocha lakini nyie wenyewe mnaweza mkaona anavyofanya maamuzi yake”amesema Pogba

Kufunguka zaidi “Unadhani nahitaji mazungumzo naye? huu sio wakati sahihi. Kama nilivyowahi kuwambia awali kuwa mimi nafanya kazi yangu, na yeye (Mourinho) anafanya kazi yake, kwani mimi nina mkataba na Manchester na ninaitumikia”.

“Unajua kuna timu, kocha lazima awe na maamuzi yake. kwa hiyo kama ataamua kuniweka benchi kwa ajili ya kiwango changu au anataka kubadili mfumo wa timu ni sahihi kwake. na ndio maana mwaka huu nimekaa benchi kwa muda mrefu.“amesema Pogba na kueleza tatizo lake na Mourinho lilikoanzia.

“Kwanini nimekaa sana benchi nilikuwa na majeraha kila mtu anajua, lakini mbaya zaidi nilipata virusi kwenye mechi dhidi ya Newcastle United. Nilitolewa kwenye mchezo kwa sababu nilipatwa na virusi na sikuwa na pumzi. Hakuna mtu aliyejua zaidi yangu na Mourinho na nisingeweza kulia mbele ya vyombo vya habari kuwa sipo sawa.“amesema Pogba.

Kwa upande mwingine Pogba amesema watu wengi wanataka kuilinganisha Man United ya sasa na ile ya zamani ya Sir Alex kitu ambacho sio sawa na kusisitiza kuwa lengo lake ni kushinda mataji yote makubwa iwe ndani ya United au nje ya klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment