Monday, June 4, 2018

Arsenal na Chelsea wameungana na Liverpool katika mbio za kuwania saini ya Golikipa wa Barcelona Jasper Cillessen, kwa mujibu wa taarifa kutoka Jarida la michezo la nchini Hispania, Sport.

Wiki iliyopita Liverpool walikuwa wakihusishwa na Cillessen na sasa wanatarajiwa kukabiliwa na ushindani kutoka kwa wapinzani wao wa Ligi kuu ya Uingereza, Arsenal na Chelsea.

Kwa mujibu wa Sport, vilabu vyote viwili vya London vimefanya mawasiliano na Mdachi huyo na wameonesha nia ya kutaka kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.

Barca hawapo tayari kumuuza Golikipa huyo wa zamani wa Ajax na wanaomuhitaji wamekumbushwa kuhusu thamani yake iliyopo kwenye mkataba wake ya Euro Milioni 60.

0 comments:

Post a Comment