Cardi B anaendelea na tabia yake ya kutetea maovu ya mume wake Offset
Cardi B amelalamikia polisi kwa kusema walipanga njama za kumkamata Offset mjini Georgia na silaha kwenye gari yake na kwamba atabaki kumtetea mume wake.
Offset alikamatwa na kufunguliwa mashtaka mawili ya kutembea na silaha kinyume na sheria, wakili wa Offset anasema polisi walisimamisha gari ya mteja wake sababu ni mtu mweusi mwenye maisha ya kifahari na hawakuwa na sababu yoyote ya kupekua gari hio.
Wakili wa Offset anasema 'Mteja wangu amekamatwa sababu ni kijana mdogo mweusi kwenye gari la kifahari akiwa amevalia vitu vya kifahari, ni kawaida kwa polisi kukamata vijana hivi wakidhani ni wahalifu'.
Offset atashinda kesi hii sababu hakuwa na silaha ila mlinzi wake ndiye alikuwa na silaha na polisi hawakuwa na sababu ya msingi ya kusimamisha gari lake.
0 comments:
Post a Comment