Wednesday, July 25, 2018


Social Media imekuwa sana hivi sasa, imekuwa ni zaidi ya mawasiliano - kwa baadhi ya watu imekuwa biashara ambazo zinaendesha maisha yao kwa kufanya matangazo ya bidhaa au huduma tofauti.

Mtandao wa HopperHQ.com, ambao unadili na masuala ya uchambuzi wa data mbalimbali za mtandao wa Instagram umetoa listi ya wanasoka watano ambao kupitia akaunti zao za instagram huenda wakawa wanatengeneza mamilioni ya fedha kwa kila post yenye kutangaza bidhaa kutokana na thamani ya akaunti zao - kwa kuangalia namba ya followers, comments na likes ambazo wanasoka hawa hupata kwenye posts zao za kila mara.

Cristiano Ronaldo mwenye followers 136m, ndio mwanaadamu wa pili kuwa na followers wengi kwenye mtandao wa Instagram (Selena Gomez 138m) - anaongoza kwenye listi ya wanasoka ambao thamani moja ya posta ya matangazo anacharge $750,000 - zaidi ya billioni 1.8billioni akifuatiwa na Neymar ambaye anacharge $600,000, Messi $500,000
:
Listi kamili ipo hivi: - Instagram Rich List
:
1. Ronaldo (136m Followers) - $750,000 (£570,000).

2. Neymar (100m Flwrs) - $600,000 (£457,000)

3. Messi (97.3m) - $500,000 (£381,000).

4. Beckham (49.7m) - $300,000 (£228,000)

5. Bale (35m) - $185,000 (£141,000

0 comments:

Post a Comment