Tuesday, July 24, 2018

RAJAB ZAHIL BEKI WA KATI

Atua Singida United akitokea Ruvu Shooting kwa mkataba wa miaka miwili.

Rajab zahili amejiunga kama mchezaji huru , amejiunga na kikosi hiki ikiwa ni pendekezo la kocha Hemed Moroco katika kuimarisha safu ya ulinzi ya Singida United kwa msimu ujao ili kufikia malengo ya club yetu.
BEKI WA KUSHOTO JAMAL MWAMBELEKO

atua Singida United kwa mkataba wa Mwaka mmoja.

Mwambeleko amejiunga na Singida United akitokea Simba S.C ambako alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja.
Maongezi mazuri kati ya Simba na Singida United yamefikia hatua ya mchezaji huyo kuelekea kwa walima alizeti kwa kukipiga msimu ujao.



KINDA ATHANASI MDAMU 

Atua Singida United kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Athanas amejiunga kama na Singida United kama mchezaji huru baada ya kumaliza masomo yake pale Alliance Academy Jijini Mwanza.Akiwa uwanjani Athanas anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati na pembeni.


0 comments:

Post a Comment