Tuesday, July 24, 2018

Matokeo ya vipimo vya afya vya Cristiano Ronaldo alivyofanyiwa na Juventus vimeonesha kwamba ana uimara wa kimwili wa kijana wa umri wa miaka 20.

Vipimo hivyo vimeonesha kwamba mwili wake una 7% ya Mafuta ya mwili ( Body Fat ) , 50% ya Uzito wa Mifupa ( Muscle Mass ) ambayo ipo juu kuliko wachezaji wenzake wenye umri kama wake.

Sio hiyo tu bali Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 alikimbia 33.98Km katika fainali za kombe la Dunia ambayo ilikuwa ni zaidi ya Mwanaume yoyote aliyecheza fainali hizo.

Kabla ya kujiunga na Juventus , jopo la Madaktari wa Real Madrid walifanya vipimo kadhaa katika mwili wa Cristiano Ronaldo na matokeo yake yalionesha kwamba ana uimara wa mchezaji mwenye umri wa miaka 23 , na sasa ukilinganisha na uimara wake ambaye ni miaka mitatu pungufu. Ajabu sana.

0 comments:

Post a Comment