Friday, July 20, 2018

Kiungo Mcongo Papi Tshishimbi amewata mashabiki wa Yanga kutowalaumu wachezaji kufuatia kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia.

Yanga imerejea jana kutoka nchini Kenya na kesho itaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa uwanja wa Taifa Julai 29 2018.

Tshishimbi amesema wakati mwingine unaposhindwa ndio unajifunza zaidi, wao walipambana kadiri ya uwezo wao.

Tshishimbi ndiye aliyen'gara kwa upande wa kikosi cha Yanga ambacho wachezaji wake wengi morali ilionekana kuwa chini.

0 comments:

Post a Comment