Kumekuwa na sintofahamu kuhusinana na mkataba wa thomas ulimwengu ndani ya klabu yake ya Al Hilal ya Sudan. Kuna taarifa zimesambaa mitandaoni kuwa Ulimwengu amevunja mkataba wake akiwa ameitumikia klabu hiyo kwa miezi mitano tu.
Meneja wa Thomas Ulimwengu Jamal Kisongo amesema, bado hana taarifa yoyote kuhusu Ulimwengu kuvunja mktaba.
"Nawaombeni muwe na subira kidogo. Jana nilitingwa na mambo mengi, bado sijawasiliana na Thomas. Leo nitakwenda msibani nadhani nikitoka nitajitahidi niwasiliane naye nifahamu hasa nini kinaendelea, kwa sasa siwezi kusema lolote."
0 comments:
Post a Comment